
anaovuta
sasa hivi unampeleka pabaya umeona eeh, tena mimi kama kaka yake
namshauri aachane na matumizi ya madawa ya kulevya kwasababu mwisho wake
utampeleka pabaya, mimi niko back stage nna show yangu nipo kazini,
tupo seious watu wa hiphop, miaka mingi tulikuwa tuna nadi amani
hatutaki matatizo na watu unaona bana, hawa ni watu ambao kwa namna moja
ama nyingine wanasababisha hiphop ishindwe kwenda mbele na kusababisha
hiphop ishindwe kwenda mbele na kuwapa mafanikio watu wa
hiphop.tumeandaa show yetu nzuri, ilikua bonge ya show moja kali ya
hiphop Tanzania kuwahi kutokea, show ambayo imekutanisha wasanii wakali
wa hiphop ambao sasa hivi wanavuma, mi niko back stage naskia sauti ya
Chidi Benz ameshika mic, muda ambao mi natakiwa kuwa stage naperfom, sa
Chidi Benz ametokea wapi mbona kwenye ratiba yetu ya show hayupo,
anaongea ubabe anakamba.yupo stage mi niko back stage bado, mi
nikawaambia watu wangu vipi, huyu mtu mbona mnamuachia anatuharibia
show? hasa watu ujue, ujue msanii, yaani jana ndio nimekubali msanii ni
mtu mwenye hadhi na heshima kubwa sana sema Chidi Benzi amejishushia
hadhi yake na heshima yake .Watu wakawa wanashindwa kumfanya kitu
wakiangalia huyu ni mtu maarufu anajulikana, watu wakawa wanamplease
kiustaarabu, Chidi eeh shuka hii show haikuhusu, sasa watu walivyokuwa
wanamplease akawa anaona labda watu mafala au nini umeona eeh.
sasa mimi kitendo kimechukua kama dakika saba au nane hivi, bado yuko tu
stage ameng'ang'ania, ananichelewesha mimi muda wa kuperfom, watu
wanataka kuona show yangu, watu wamelipa hela zao, wameacha shughuli zao
waje kumuona kalapina, ye anataka kuzkwaza watu wasimuone Kala pinia,
huyu mtoto si adui jamani......." amesema Kala Pina ..endelea
kumsikiliza hapo chini
baada ya kuzungumza hayo Chidi aliandika haya kwenye ukurasa wake wa facebook
"Siku
moja professa J alipanda stage Bilz mimi napafom,kwa furaha zake na
akanipora mic na kuanza kuchana ngoma zangu.watu wakajua nitamsukuma au
kumpiga kutokana na aliyokua anayafanya pale.kama broza sikumfanya
chochote..nilijua mizuka ya kisanii.tulimaliza show na tukaendelea na
story. Hakuna Ubaya mpk Uutengeneze ubaya.peace"